U.S. Embassy Dar es Salaam

TANZANIA




By U.S. Ambassador to the United Republic

of Tanzania Michael A. Battle Sr.


May 2, 2024 - Since 1993, thanks to a UNESCO General Conference recommendation, World Press Freedom Day has been commemorated globally on May 3rd.  This year, I am honoured to participate in the official commemoration in Dodoma alongside government officials, international partners, and civil society leaders.  These events underscore the pivotal role of press freedom in fostering vibrant democracies by enabling citizens to make well-informed decisions and holding governments and their leaders accountable to the public.


In the United States, we cherish an informed citizenry as the bedrock of democracy, which is why freedom of speech and the press are safeguarded in the First Amendment of the U.S. Constitution. 


My tenure as U.S. Ambassador to Tanzania has been profoundly enriched by engaging with journalists from all backgrounds.  Citizen journalists, with their unique vantage points, can change the trajectory of a nation, and the professionalism of trained journalists remains important for accurately framing the national debate.  Collectively, their work vividly illustrates how a free press combats ignorance—the foremost of the three adversaries identified by Mwalimu Julius Nyerere—and empowers society.


Yet, the power of information hinges on the quality of the underlying data. On this World Press Freedom Day, I want to highlight the excellent work of AidData, a data research lab based at the College of William & Mary in the United States. Today, AidData released a report
assessing the value of the U.S.-Tanzanian partnership for the Tanzanian people.  


The United States collaborates extensively with Tanzania, supporting a range of initiatives, from health and capacity-building efforts to democratic governance. Yet, to really understand the value of that partnership, accessible data is necessary. 


AidData’s mission to enhance the transparency of development finance is crucial. By providing journalists worldwide with accessible, detailed data on how and where assistance funds are allocated, AidData empowers the press and the public to effectively hold governments and international entities accountable. All citizens should have access to open data to assess the efficiency and impact of investment on local communities.


At a macro level, AidData’s reporting finds that the United States, through government agencies, organisations, and individuals, contributes an estimated $2.8 billion annually (TZS 7,140 Bn) to Tanzania’s development.  We have also opened our doors to Tanzanians to live, work, and study in the United States.  The Tanzanian diaspora contributes an additional $96.4 million to the Tanzanian economy annually through remittances from the United States.  The United States, as the single largest donor to HIV/AIDS prevention and treatment over the last 20 years, has prevented the premature deaths of roughly 750,000 Tanzanians. 


With access to open data, AidData has done the hard work of quantifying the impact of the U.S.-Tanzania partnership on all Tanzanians. This data tells a story, enabling the people of Tanzania to make informed choices about how best to engage with partner nations to achieve their national development goals. I hope everyone will take the time to read this report and assess how the U.S.-Tanzania partnership impacts their daily lives.


President Samia Suluhu Hassan said during Vice President Kamala Harris’s visit last year, “We have endeavoured to build a democratic state that upholds transparency and respect of the rule of law.”  We support the President’s vision and will continue to work tirelessly with like-minded Tanzanians across government and civil society to make that vision a reality for all Tanzanians. 


Today, I join Americans, Tanzanians, and people across the globe as we defend the freedom of the press and support informed citizenries.  There is no freedom in a society without a free press, and we guard that sacred right today and every day. 


Na Mwandishi Wetu, Arusha

WATU zaidi ya 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) na kati yao kubainika kuwa wana tatizo la uzito uliopitiliza.

Pia kati ya watu hao hakuna aliyebainika kuwa na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU), lakini mmoja amekutwa na dalili zote za kifua kifuu hivyo kupewa rufaa ya kwenda katika Hospitali ya Mount Meru iliyopo mkoani humo.

Hayo yamebainishwa na Daktari wa GGML aliyebobea katika magonjwa yatokanayo na kazi, Cretus Karwan alipozungumza na mwandishi wetu kuhusu huduma za afya zilizokuwa zinatolewa kwenye banda la GGML katika maonesho ya afya na usalama kazini (OSHA) 2024 yaliyofanyika jijini Arusha.

Alisema katika banda hilo wameendelea kupima uzito, urefu na magonjwa mbalimbali kama vile kisukari, shinikizo la damu, VVU na magonjwa mengine.

“Mathalani kuna binti mmoja tulimpima tukakuta presha na sukari yake imeshuka na tulibaini ni kutokana na kwamba kutokula kwa wakati. Alikuja mchana hivyo tulimpa huduma ya kwanza na kumshaui aende kunywa supu na maji mengi,” alisema.

Alisema pamoja na mambo mengine washiriki au wananchi waliotembelea banda la GGML pia walijifunza namna kampuni hiyo inavyotoa huduma za afya kwa wanyakazi wake.

“Washiriki au wateja wetu tuliwaeleza tunachofanya tunapokuwa kazini. Tuliwaeleza tunamfanyia vipimo mfanyakazi anapoajiriwa kujua kwamba kwa kazi aliyoajiriwa anaimudu au lah kulingana na afya yake kabla ya kufanya kazi na GGML.

"Hivyo tunampima pia kuainisha uzito na urefu ulivyo na kumshauri. Tunapima masikio, macho, kifua na vitu vingine kujua yuko sawa au lah. Hivi ni vipimo ambavyo kila mwaka huwa tunarudia,” alisema.

Pia alisema huwa wanapima eneo la kazi la mfanyakazi kujua kama kiwango cha kelele kimezidi, vumbi na vitu vingine ili kujua kama mfanyakazi ameathirika.
“Haya ni matakwa ya kisheria kwamba mtu anapofanya kazi katika mazingira fulani tunamdhibitishia ameathirika au lah na wao wanakuwa na amani.

“Hii inatusaidia kwa sababu mtu akiacha kazi, au kustaafu pia tunampima ambapo yeye binafsi anajua tangu alipoingia mgodini ameathirika na tatizo lolote au lah lakini pia na mgodi unajua ameondoka yuko vizuri au lah,” alisema.

Alisema iwapo mfanyakazi akikutwa na tatizo lolote anaelekezwa sehemu husika ambapo ni mfuko wa fidia kwa wafanyakazi hivyo mtu huyo anafaidika.

Mmoja wa wananchi waliojitokeza kupata huduma za afya kwenye banda hilo, Mussa Abdalah aliishukuru kampuni hiyo kwa kutoa huduma hizo kwani mbali na wananchi kupata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu afya na usalama mahali pa kazi, pia imekuwa fursa kwao kujua hali ya afya zao bure.

“Hivi ni vipimo vya bure kabisa, ukienda hospitali lazima mfuko utoboke lakini hapani bure. Kwa kweli tunashukuru sana kwa huduma hii,” alisema Abdallah ambaye ni mkazi wa Moshono mkoani humo.



 

 Daktari wa GGML aliyebobea katika magonjwa yatokanayo na kazi, Cretus Karwan akimpatia vipimo mmoja wa wananchi waliotembelea banda la GGML na kupatiwa huduma za awali za upimaji wa afya katika maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Arusha.

Na Mwandishi Wetu

SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) pamoja na Wakala wa Usalama na Afya mahalipa kazi (OSHA) wametoa mwito kwa kampuni nyingine za madini kuiga mbinu na na miongozi inayotumiwa na Geita Gold Mining Limited (GGML) katika kuzingatia kanuni za afya na usalama mahali pa kazi.

Mwito huo umetolewa kwa nyakati tofauti na viongozi wa taasisi hizo waliotembelea banda la GGML katika maonesho ya Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa kazi (OSHA) yanayoendelea kwenye viwanja vya General jijini Arusha.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya OSHA, Dk. Adelhelm Meru alisema kinachooneshwa na GGML katika maonesho hayo kimedhihirisha ni kwa namna gani kampuni hiyo inaungana na serikali katika kudhibiti majanga migodini.

Alisema teknolojia hizo zinazohusu vifaa mbalimbali ikiwamo kifaa maalum cha ProLaser Speed Gun ni mifano michache ambayo inaweza kuigwa na kampuni nyingine katika kulinda afya na uhai wa wafanyakazi wao ajali zinazotokana na mwendo kasi

Naye Rais wa TUCTA, Tumaini Nyamhoka alieleza kufurahishwa na teknolojia zinazotumiwa na GGML katika utekelezaji wa majukumu yake kwani zimekuwa chanzo cha wafanyakazi kufanya kazi katika mazingira rafiki na salama kwao na kwa familia zao.

“Ninatamani viongozi wakubwa wanaoendelea kutembelea maonesho haya wapite katika banda ya GGML wajionee wenyewe teknolojia hizi tunazozingumzia,” alisema.

Alisema teknolojia hizo ni za kipekee na zinalenga kutekeleza kwa vitendo tunu ya kampuni hiyo ambayo ni afya na usalama mahali pa kazi.

Shughuli za Mgodi wa Dhahabu wa Geita zinahusisha uendesha wa mitambo mikubwa, malori na magari.

Kifaa hicho cha ProLaser Speed Gun kilichokuwa kinatumika kuelimisha washiriki wa maonesho hayo, husaidia kudhibiti mwendo kasi wa magari na kupunguza ajali.

Mratibu wa Usalama, Walter Marealle alifafanua kwa kutumia kifaa hicho GGML huweza kufutilia mwendo kasi wa magari ndani ya kampuni na kuwawajibisha madereva ambao hawazingatii taratibu.

Alisema kifaa hicho kinasaidia kupunguza ajali, majeraha na vifo hivyo kuendelea kuwaweka wafanyakazi katika hali ya usalama.

“Data zilizokusanywa na ProLaser Speed Gun pia inasaidia GGML kutambua maeneo ambayo mwendokasi ni tatizo na kuandaa hatua zinazolstahili kushughulikia suala hilo.

" ProLaser Speed Gun ni sehemu moja tu ya hatua zinazochukuliwa na GGML kuzingatia afya na usalama mahali pa kazi. GGML pia inatumia alama za wazi na alama za barabarani kumkumbusha kila mtu juu ya ukomo vya mwendo kasi na kutoa mafunzo ya udereva ili kuwapa waendeshaji wake maarifa na ujuzi muhimu wa kufanya kazi kwa usalama,” alisema.
 

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhoka akipokea zawadi kutoka kwa Ofisa Mwandamizi wa masuala ya jamii na maendeleo ya kiuchumi kutoka GGML, Ruth Mharagi alipotembelea banda la GGML katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi jijini Arusha.
Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhoka pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya OSHA, Dk. Adelhelm Meru wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa GGML.viongozi hao walitembelea bandala GGML katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Usekelege Mpulla (kushoto) na Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji  Tanzania (TIC)  Gilead Teri, wakipeana mikono baada ya kumaliza kusaini mkataba wa makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja ili kusuluhisha kwa haraka migogoro  ya kazi na kuruhusu wawekezaji kufanya kazi zao za ukuzaji uchumi wa nchi. Hafla ya makubaliano hayo imefanyika leo Mei 2,2024 jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia kulia na kushoto ni wanasheria.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Usekelege Mpulla ( kushoto) na Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji  Tanzania (TIC)  Gilead Teri, wakisaini mkataba wa makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja ili kusuluhisha kwa haraka migogoro  ya kazi na kuruhusu wawekezaji kufanya kazi zao za ukuzaji uchumi wa nchi. Hafla ya makubaliano hayo imefanyika leo Mei 2,2024 jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Usekelege Mpulla (kushoto) na Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji  Tanzania (TIC)  Gilead Teri, wakibadilisana mikataba mara baada ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja ili kusuluhisha kwa haraka migogoro  ya kazi na kuruhusu wawekezaji kufanya kazi zao za ukuzaji uchumi wa nchi. Hafla ya makubaliano hayo imefanyika leo Mei 2,2024 jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia kulia na kushoto ni wanasheria.
Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji  Tanzania (TIC)  Gilead Teri akizungumza wakati wa hafla ya kusaini  mkataba wa makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja ili kusuluhisha kwa haraka migogoro  ya kazi na kuruhusu wawekezaji kufanya kazi zao za ukuzaji uchumi wa nchi. Hafla ya makubaliano hayo imefanyika leo Mei 2,2024 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Usekelege Mpulla akizungumza wakati wa kusaini mkataba wa makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja ili kusuluhisha kwa haraka migogoro  ya kazi na kuruhusu wawekezaji kufanya kazi zao za ukuzaji uchumi wa nchi. Hafla ya makubaliano hayo imefanyika leo Mei 2,2024 jijini Dar es Salaam.

KATIKA kuhakikisha mazingira bora kwa wawekezaji nchini Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) wamesaini makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja ili kusuluhisha haraka migogoro ya kazi na kuruhusu wawekezaji kufanya kazi zao ukuzaji uchumi

Makubaliano hayo yamesainiwa leo Mei 2, 2024 na pande zote mbili huku upande wa TIC ukiwakilishwa na Mkurugenzi wake Mtendaji Gilead Teri na upande wa CMA ukiwakilishwa na Mkurugenzi Mkuu wake Usekelege Mpulla huku wakurugenzi hao wote wakikiri kuwa hilo ni gaizo la Rais Samia Suluhu Hassan

Teri amesema kuwa Taasisi hizo zimeungana kuhakikisha mwekezaji anapata mazingira mazuri ya kufanya shughuli zake.

"Naomba nieleweke kuwa sio wawekezaji wa nje tu wanaopata changamoto hata wa hapa ndani hivyo tunatekeleza agizo la Rais juu ya kuhakikisha wawekezaji wanapotaka kuwekeza wafanye kazi zao kwa misingi ya sheria pasipokuwa na uonevu".

"Palikuwepo na hisia kwamba baadhi ya mifumo na sheria zinatoa mianya kwa baddhi ya wawekezaji kuonewa eneo moja wapo katika utatuzi na usuluhishi wa migogoro kati ya wawekezaji na waajiriwa" amesema Teri.

Ametanabaisha kuwa jitihada hizo hazikufanywa na TIC isipokuwa ni msukumo wa Mkurugenzi wa CMA , Mpulla ambaye alifika TIC kwa ajili ya kujadili nia ya kumaliza tatizo hilo.

"Jitahada hizi zimetoka kwa ndugu yangu Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), na yeye ndiye aliyetutafuta akisema hatutaki wawekezaji wenu wakija suala la usuluhishi liwe changamoto kwao wakija kuwekeza, naomba nikupongeze sana ndugu yangu, wewe pamoja na timu yako yote kwa kuona umuhimu wa kushirikiana na TIC ili kuhakikisha kwamba mazingira ya uwekezaji nchini yanakuwa rafiki" amesema Teri.

Amesema kuwa Taasisi hizo zimekubaliana mambo mengi lakini mambo mawili ndio msingi tumekubaliana mambo mengi lakini ya msingi niol mawili.

"Jambo la kwanza tulilokubaliana kushirikiana CMA na TIC ni kukuza uelewa wa masula ya usuluhishi na uamuzi wa migogoro ya watumishi au wafanyakazi tungependa wawekezaji wote wafahamu sheria za hapa nchini , haki zao na wajibu wao kwenye eneo hili tutahakikisha kila mwekezaji anazijua "

"Eneo la pili ni kukuza majadiliano katia ya wewekezaji kaytia CMA, TIC na wawakilishi wa Wafanyakazi lengo lake kabla changamoto zikafika hatua mwekezaji hajapigwa faini kubwa kuwe na namna ya majadiliano kwa pamoja katia ya CMA na TIC bila kuathiri sheria zote mbili." amesema Teri.

Teri amesema Taasisi hizo zinatekeleza adhma ya rais mwekezaji yoyote awe wa ndani au kutoka nje asikutane na vikwazo vitakavyomrejesha nyuma kwenye uwekezaji wake muhimu umma ufahamu uwekazaji na ajira ni pande mbili za sarafu moja pakitokea uwekezaji wanafaika namba moja ni Watanzania wanaoajiriwa.

Kwa upande wake, Mpulla amesema kuwa CMA imebeba jukumu hilo ili kupunguza msongamano wa mashauri ya migogoro kazini "tulijiona tunawajibu wa kuunga mkono juhudu za Rais kwenye kuvutia uwekezaji nchini tumeona anakwenda huku na kule kuwavuta waje sasa hawa wanaokuja sisi tunawajibu wa kuwahuduma vizuri ili waambiane waje": .

"Majukumu yetu makuu ni utatuzi wa migogoro ya kazi kwa njia ya usuluhishi na uamuzi tunajukumu la kisheria na kwamba sheria ya ajira na mahusiano kazini lengo kuu ni kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia haki jamii kama kuchochea ukuaji wa uchumi na wenzetu TIC wanamalengo hayo hayo kwa hivyo hiyo ndio sababu ya kuungana nao" Amesema Mapulla.

Mapulla amesema uwekezaji unachochea ajira ilhali ajira zinakuwa zinamigogoro "Kadri wawekezaji wanavyokuja nchini ndivyo fursa za ajira zinavyoongezeka kadri fursa hizo zinavyoongezeka basi uwezekano wa kutokea migogoro ya kikazi ni mkubwa na sisi tunapaswa kuingia hapo kumhakikishia mwekezaji kwamba iwapo itatokea migogoro yab kikazi katika nchi yetu basi MCA tutahakikisha tunatengeneza amani sehemu ya kazi kwa hivyo tunawajibu wa kuwahakikishia wawekezaji kuwa migogoro inatatuliwa kwa wakati na kwa haki na kuhakikisha wanatumia muda mwingi kuzalisha na kukuza uchumi kuliko kutumia muda mwingi kwenye migogoro" amesema .

MATUMIZI ya njia mbalimbali za uzazi wa mpango yameongezeka katika Zahanati ya Ubinga Kijiji cha Ubinga wilayani Nzega mkoani Tabora ambapo kwa wiki wanahudumia wahitaji 100 kutoka 40 kwa mwaka 2021.

Wakati kukiwa na ongezeko hilo, mkakati wa serikali kupitia Wizara ya Afya katika matumizi ya uzazi wa mpango kwa mwaka 2019/2023 ulikuwa unakadiriwa kupunguza mimba zisizotarajiwa 7,148,748, utoaji mimba holela 2,669,638 na vifo 22,164.

Ongezeko hilo la matumizi ya uzazi wa mpango katika kijiji hicho cha Ubinga umetokana na uhamasishaji uliofanywa na Shirika lisilo la Kiserikali la Maria Stopes Tanzania kupitia mradi wake wa kuimarisha vituo vya umma (Public Sector Streghtening-PSS ) kuwawezesha wahudumu wa afya kupata elimu na kuwajengea uwezo na kuwezesha upatikanaji wa njia za uzazi wa mpango.

Akizungumza na Michuzi Blog, Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Ubinga, Raphael Peter amesema mafunzo yaliyotolewa na Maria Stopes kupitia mradi wake wa PSS yameleta tija kwa jamii yao.

Amesema, tangu wahudumu wapate mafunzo ya utoaji huduma ta uzazi wa mpango na kuwezeshwa vifaa, huduma hizo zimekuwa zikifanyika kila siku katika zahanati hiyo tofauti na hapo mwanzo ambapo huduma zilifanyika mara moja kwa mwezi.

“Siku za nyuma huduma hizi hazikutolewa kwasababu watoa huduma walikuwa hawana ujuzi huu vizuri, kwahiyo tulianza kuhamasisha kupitia wahudumu wetu waliopo kwenye jamii wateja wakaanza kuongezeka namba iliongezeka na zaidi namba hiyo inajieleza kwenye vitabu kulingana na takwimu zilizopo kwenye mifumo ya afya” amesema Dk Peter

Amesema kituo cha Ubinga kimenufaika kwa kiwango kikubwa kwa kupata vitendea kazi vya mara kwa mara na kutembelewa na wadau wengi hivyo kufanya huduma za uzazi wa mpango kuwa hai huku akitaja changamoto kubwa kuwa ni kuwa na muitikio mdogo kwa upande wa akina baba.

Kwa upande wake Muuguzi na Mkunga katika zahanati ya Ubinga Aziza Simangwa amesema kumekuwa na changamoto kubwa ya imani potofu ambapo zinaletwa na maneno ya mtaani na kupotosha watu kuhusu matumuzi ya uzazi wa mpango.
Na Janeth Raphael -MichuziTv -Dodoma

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Raisi wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Dkt Tulia Ackson amaetoa Rai kwa Waandishi wa habari na Watangazaji Nchini kutumia muda wao kuandika na kuhabarisha Umma kuhusiana na Mazingira pamoja na Mabadiliko ya tabia ya Nchi.

Dkt Tulia ameyasema hayo mapema Leo hii May 2 Jijini Dodoma wakati akifungua Kongamano la wana habari kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa vyombo vya habari Duniani ambayo hufanyika May 3 kila mwaka.

"Nitoe Rai kwa Waandishi wa habari na Watangazaji kutumia muda wenu kuandika habari za kuhabarisha Umma kuhusiana na mazingira na mabadiliko ya tabia ya Nchi,hasa katika kipindi ambacho tunakipitia ambacho wakati mwingine sio mara zote watu huusisha na kila jambo linalotokea katika jamii ili mradi nila mazingira basi tunalihusisha na mabadiliko ya tabia ya nchi,Tunawategemea sana katika kuhabarisha na kuelimisha Umma kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi ".

Aidha Dkt Tulia amesema kuwa takwimu za Watafiti zinaonesha kuwa takribani watu milioni 16 nchini Tanzania wanategemea rasilimali za pwani kwaajili ya kuendesha maisha yao hivyo uharibifu ukitokea unaathiri hao watu wote milioni 16 hivyo wasimame hapo kuokoa mazingira pia".

"Takwimu za watafiti zinaonesha kuwa takribani watu milioni 16 nchini Tanzania wanategemea rasilimali za pwani kwaajili ya kuendesha maisha yao,na kwahiyo uharibifu wote unaotokea unahatarisha maisha ya hao watu milioni 16, Katika Muktatha huo tunawagemea Waandishi wa habari kusaidia kuokoa haya mazingira ambayo na ninyi kwa kuona umuhimu wake tunaamjni mtafanya uchunguzi lakini pia ninyi mmeweka kwenye kauli mbiu yenu kuonesha kwamba mtashiriki pamoja na sisi kwenye jambo hilo".

Awali akimkaribisha Mgeni Rasmi, Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe Nape Nnauye yeye amesema kuwa kazi ya vyombo vya habari hapa Nchini ni nzuri hata kama hatujafika tunakokutaka lakini tumepiga hatua sana katika sekta hii.

"Kwa kifupi niseme kazi ya ya vyombo vya habari ni nzuri hapa Nchini kama nilivyotangulia kusema, inawezekana hatujafika tunakotaka kwenda lakini tumepiga hatua kubwa na tunaendelea kusonga mbele na Serikali ya awamu ya 6 chini ya usimamizi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameruambia tuache milango wazi kila tunapohitajika na kila panapohitajika kufanya marekebisho ya hapa na pale".

Kongamano hili limehudhuriwa na wadau wa Sekta ya Habari Nchini wapatao 300 wakiongozwa na Kauli mbiu isemayo:Uandishi wa habari katikati ya Changamoto za Mazingira.






Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe amebainisha mikakati ya serikali katika kuongeza uzalishaji wa zao la Mkonge kutoka tani 56,732.69 mwaka 2023/2024 hadi tani 80,000 mwaka 2024/2025.

Akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka 2024/2025, Mhe. Bashe amesema Wizara yake kupitia Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) lengo hilo litafikiwa kwa kununua zana za kilimo kwa ajili ya kuwezesha uendelezaji wa mashamba makubwa ya pamoja na kununua mashine ya kuchakata mkonge (korona).

“Pamoja na mambo mengine, tutaendeleza miundombinu ya kituo cha uchakataji cha Handeni, kukarabati miundombinu ya shamba la Kibaranga na kuwezesha umiliki wa ardhi ya kilimo yenye ukubwa wa hekta 6,000 kwa ajili ya kuanzisha mashamba makubwa ya pamoja katika mikoa ya Tanga, Singida na Morogoro.

“Aidha, Bodi itaratibu usambazaji wa miche ya Mkonge milioni tatu katika maeneo ya uzalishaji na kupitia TARI itatoa mafunzo kuhusu uzalishaji wa Mkonge na fursa zitokanazo na zao hilo kwa wadau 100,000 na maafisa ugani 500,” amesema Mhe. Bashe.

Mhe. Bashe amesema katika kuongeza matumizi ya mmea wa Mkonge, Bodi kwa kushirikiana na Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela (NM-AIST), itajenga kituo cha uzalishaji wa Inzi chuma (black soldier flies) kwa kutumia mabaki ya Mkonge (Sisal waste) ili kutengeneza protini kwa matumizi ya binadamu na mifugo (wanyama, ndege na samaki).

“Pia, Bodi itawezesha utafiti wa zao la Mkonge utakaofanywa na watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), TARI-Mlingano, Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela (NM-AIST) kwa kushirikiana na Kampuni ya Carbonovia UK ya Oxford Uingereza kuhusu uwezekano wa kuzalisha protini kutokana na hewa ukaa (Carbon dioxide) kutoka kwenye mabaki ya Mkonge.

“Aidha, Bodi kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza na Chuo cha Mafunzo Zanzibar itaanzisha na kuimarisha utaalamu wa uzalishaji wa bidhaa za mikono za Mkonge ili kutengeneza ajira kwa vijana na wanawake,” amesema Mhe. Bashe.
Na Janeth Raphael -MichuziTv -Dodoma

Katika kuelekea kilele cha Siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari ambayo huadhimishwa May 3 kila mwaka Duniani suala la akili mnemba limeendelea kujadiliwa kwa upana kwa faida na hasara zake ambapo moja ya faida zake imeelezwa kuwa ni kuleta utambuzi wa mbolea gani inaweza kufaa katika eneo lipi hapa Nchini ili badala ya kuwa mbolea aina moja hivyo itaweza kutambua na kuwa nambolea tofauti tofauti.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwanzilishi wa NGO's ya Omuka Hub Neema Lugangira katika moja ya mijadala iliyokuwa ikiendelea katika shamla shamla za kuelekea Maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari Duniani inayofanyika Jijini Dodoma.

"Tunapoongelea akili mnemba kuna faida nyingi sana hakuna ambaye anaweza kupinga kwamba ina faida sana, tukichukulia mfano katika Sekta ya kilimo kwa kutumia akili mnemba tunaweza tukatambua labda ni mbolea gani ainaweza kufaa eneo gani la nchi ili badala ya kununua aina moja ya mbolea ambazo tunanunua kulingana na maeneo husikahiyi ni moja ya faida. Lakini hata katika Sekta ya Afya kuna faida zake,hata kwa wanafunzi kufanya tafita zao"

Sambamba na hayo pia Neema amaeleza Changamoto za hiyo akili mnemba kuwa ni pamoja na utoaji wa taarifa zisizo sahihi yaani upotoshaji wa Taarifa na kutoa mfano kilichotokea kwa Raisi wa Zambia mwaka ambapo clip ilisambaa ikisema kuwa Raisi huyo hatagombea tena Uraisi na vyombo vya habari vikaamini hivyo mpaka pale Ofisi ya Raisi ilipokanusha kuwa clip hiyo haina ukweli.

"Lakini pia kila lililo jema lina upande wake mwingine akili mnemba inachangamoto zake nyingi sana na changamoto hizi zisipotiliwa mkazo au maanani hata zile faida zitakuwa hazina maana".

"Katika changamoto zilizopo moja ni upotoshaji wa wa taarifa,Mfano mwaka jana Raisi wa Zambia ilitoka Video Clip yake ikisema kuwa yeye hatogombea tena Uraisi ilikuwa video ambayo ukiitizama unaona yeye kasema,ikaoneshwa kila mahali na hata vyombo vikubwa wakaichukua na kuiweka, lakini baadae Ofisi ya Raisi waksema si kweli na kuwa imetengenezwa sasa fikiria taharuki iliyokuwa imetokea hapo".

Pia amezungumzia masuala ya ukatili kwa wanawake na akili mnemba hasa katika kipindi hiki tunachoelekea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Hata Uchaguzi Mkuu wa 2025 kuwa waathirika wakubwa watakuwa ni Wanawake katika Siasa.


"Na hivi tunavyoelekea kwenye Uchaguzi nadhani kuna umuhimu mkubwa sana wa Wanahabari kabla ya habari kutoka,kuichapisha na kuisambaza kuhakikisha kwamba hii habari ni kwelie. Kwasababu inaweza kuzua taharuki kubwa sana".

"Lakini ukija katika eneo lingine ni kwenye ukatili wa kijinsia wa wanawake hasa linapokuja suala la matumizi ya teknolojia kwa bahati mbaya sana kati ya waathirika wakubwa ni sisi wanawake katika Siasa,kwani sisi soye sauti zetu zinajulikana video clip zetu zipo kwahiyo mtu anaweza akachukua maneno utafikiri wewe ndo umeyasema kumbe hujawahi kusema. Lakini mbaya zaidi uanweza ukatengenezewa kitu cha ajabu kwamba uko na mtu fulani na mkifanya jambo fulani na Uchaguzi ndo katikati umewaka moto,sasa kwa jambo hilo kwenye Uchaguzi itakuwaje,kwahiyo kunwa mambo lazima kayaangalia mapema".

Naye Harold Sungusia wakati akichangia Mada hiyo ya matumizi ya akili mnemba amesema kuwa katika changamoto hizo tusikate tamaa kwani anaamini pamoja na changamoto kuonekana kuwa nyingi lakini tukijipanga tunaweza fanya vizuri katika eneo hilo.

"Kitu ambacho nilikuwa najaribu kupendekeza kwenye hizi changamoto ni tusikate tamaa,lakini naamini kwamba tukijipanga vizuri bado tukafanya vizuri,kwasbabu tayari tunao Watanzania wanaofanya vizuri.Mfano kwenye Sekta ya afya,Sekta imetoa muongozo wa matumizi ya akili mnemba katika sekta afya Nchini na Imeonesha kusapoti vijana na vikundi mbalimbali kubadili matuzimi mabaya ya akili bandia na kuwa matumizi mazuri".

Kwa upande wake Nuzulack Dausen ambaye ni Mtendaji Mkuu Nukta Afrika amesema kuwa akili mnemba katika sekta ya habari inatumika katika uchakataji wa habari yani kuanzia kukusanya habari hizo,tofauti na zamani kulikuwa hakuna hiko kitu.

"Kwenye sekta hii ya habari akili mnemba inatumika katika mfumo wa uchakataji wa habari kwamba kuanzia kukusanya habari,zamani tulikuwa tulitumia maiki na kwenda kuchakata Radioni lakini saizi tunaweza kutumia akili mnemba kufanya hicho kitu".





Benki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta ya fedha na bima kama mshindi wa pili (first runner up) katika tuzo zilizotolewa na Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) wakati wa kufunga Wiki ya Maadhimisho ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi 2024 yaliyofanyika jijini Arusha.

Mgeni Rasmi katika hafla ya utoaji tuzo alikua Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) - Mhe. Deogratius Ndejembi aliyeambatana na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Patrobas Katambi.

Maadhimisho haya hujumuisha shughuli mbali mbali zinazolenga kuendelea kuhamasisha uzingatiaji wa masuala ya Usalama na Afya mahali pa kazi hapa nchini. Na benki ya NMB iliweka banda katika viwanja vya ndndndn kuonyesha dhamira na hatua wanazozichukua kuhakikisha wanadhibiti athari za mabadiliko ya tabia nchi katika shughuli zao.




KAIMU Mganga Mkuu wa Serikali Ziada Sellah,akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa mwaka pamoja na kusherehekea mafanikio ya Mradi wa kuboresha mafunzo na huduma za famasi nchini (MAP-QPS) awamu ya pili uliokwenda sambamba na uzinduzi wa mifumo ya TEHAMA na ugawaji wa vitabu vya Famasi jijini Dodoma.


Mkurugenzi Mtendaji wa CSSC, Peter Maduki,akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa mwaka pamoja na kusherehekea mafanikio ya Mradi wa kuboresha mafunzo na huduma za famasi nchini (MAP-QPS) awamu ya pili uliokwenda sambamba na uzinduzi wa mifumo ya TEHAMA na ugawaji wa vitabu vya Famasi jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa huduma za Afya kutoka Christian Social Services Commission (CSSC) Dkt.Josephine Balati,akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa mwaka pamoja na kusherehekea mafanikio ya Mradi wa kuboresha mafunzo na huduma za famasi nchini (MAP-QPS) awamu ya pili uliokwenda sambamba na uzinduzi wa mifumo ya TEHAMA na ugawaji wa vitabu vya Famasi jijini Dodoma.
Mkuu wa Miradi, Ukanda wa Afrika kutoka shirika la action medeor e.v,Bi.Susanne Schmitz,akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa mwaka pamoja na kusherehekea mafanikio ya Mradi wa kuboresha mafunzo na huduma za famasi nchini (MAP-QPS) awamu ya pili uliokwenda sambamba na uzinduzi wa mifumo ya TEHAMA na ugawaji wa vitabu vya Famasi jijini Dodoma.


Baadhi ya Washiriki wakimsikiliza Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Ziada Sellah (hayupo pichani),wakati wa mkutano mkuu wa mwaka pamoja na kusherehekea mafanikio ya Mradi wa kuboresha mafunzo na huduma za famasi nchini (MAP-QPS) awamu ya pili uliokwenda sambamba na uzinduzi wa mifumo ya TEHAMA na ugawaji wa vitabu vya Famasi jijini Dodoma.

KAIMU Mganga Mkuu wa Serikali Ziada Sellah,akigawa vitabu mara baada ya kuzindua zoezi la ugawaji wa vitabu vya Famasi jijini Dodoma.

KAIMU Mganga Mkuu wa Serikali Ziada Sellah,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua mkutano mkuu wa mwaka pamoja na kusherehekea mafanikio ya Mradi wa kuboresha mafunzo na huduma za famasi nchini (MAP-QPS) awamu ya pili uliokwenda sambamba na uzinduzi wa mifumo ya TEHAMA na ugawaji wa vitabu vya Famasi jijini Dodoma.

Na.Mwandishi Wetu

Shirika la Christian Social Services Commission (CSSC) kwa kushirikiana na shirika la action medeor e.v la nchini Ujerumani wamefanya mkutano wa mwaka ambao umewakutanisha wadau wa famasi nchini Jijini Dodoma.

Kwa pamoja wameshiriki kujadili mafanikio mbalimbali yaliyopatikana kwa kipindi cha miaka mitatu ya awamu ya pili ya mradi wa Multi-actors Partnership for Quality Pharmaceutical services (MAP-QPS).

MAP-QPS ni mradi unaoshirikisha wadau mbalimbali wenye lengo la kuboresha huduma za kifamasia Tanzania. Baadhi ya wadau ni CSSC, action medeor e.v, Wizara ya Afya, Baraza la Famasi, Vyuo vya famasi (vyuo vya kati na vyuo vikuu), Chama cha Wafamasia, Chama cha wanafunzi wa famasi, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya ufundi stadi, Tume ya vyuo vikuu, Hospitali za mikoa na Hospitali za Rufaa naTawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Mafanikio ambayo yamepatikana katika awamu ya pili ya mradi huu ni: kuboresha mafunzo ya famasi Tanzania, kutengeneza mfumo wa TEHAMA kwa ajili ya kutathmini na kuboresha mafunzo (CQIMS), kutengeneza jukwaa la kidigitali (Digital Learning Platform-DiLPHAS), kwa ajili ya kurahisisha kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa famasi kutoa mafunzo ya huduma tabibu za kifamasia (Clinical Pharmacy Services) kwa wafamasia wafanyakazi katika hospitali 29 zikiwemo za kanda, mikoa, rufaa na hospitali za kibingwa, kutoa mafunzo ya mbinu za ufundishaji (Teaching Methodology and Assessment) kwa wakufunzi 200 wa vyuo vya kati vya famasi, kukarabati na kutoa vifaa vya maabara kwa chuo cha Afya na sayansi shirikishi Mpanda, kuboresha miundombinu na kutoa vifaa vya maabara ya chuo kikuu cha RUCU, Kuwezesha kufanyika mapitio ya mitaala ya Famasi na kwezesha upatikanaji wa vitabu 1800 vya rejea kwa vyuo vinavyotoa mafunzo ya famasi.

Sambamba na hayo, Mkutano huu umezindua rasmi mfumo wa TEHAMA kwa ajili ya kutathmini na kuboresha mafunzo katika vyuo vya afya nchini.

Aidha katika mkutano huu, CSSC imetoa vitabu vya ziada vyenye thamani ya shillingi Milioni 68 vilivyoandaliwa kwa ajili ya mafunzo ya famasi. Vitabu hivyo vimegawiwa kwa vyuo takribani 100 vinavyotoa mafunzo ya famasi.

Akiongea wakati wa kukabidhi vitabu hivyo mkurugenzi wa CSSC, Peter Maduki alisema, “Vitabu hivi vimenunuliwa kutoka kwa waandishi wazawa wa nchini kwetu Tanzania na vitanufaisha wanafunzi wa kada ya famasi na vitawasaidia kuongeza ujuzi na uelewa wao wa masomo ya famasi ili kuboresha viwango vya mafunzo na wataalamu bora wa famasi.”

Akikabidhi vitabu hivyo Naibu Mganga Mkuu wa Serikali, Ziada Sellah amesema “ Wakufunzi na wataalamu wa famasi tuendelee kuongeza ujuzi wetu ili tuweze kufanya kazi kwa uweledi na tuchangie ukuaji wa sekta ya afya.”

Katika kipindi cha miaka mitatu ijayo mpaka 2026 tunaingia katika awamu ya tatu ya Mradi ambao tutashirikiana na Chuo Kikuu Cha sayansi na Afya shirikishi cha Muhimbili kutoa mafunzo na kuwajengea uwezo wafamasia waliopo kwenye ajira kwenye hospitali za kanda, rufaa na maalumu ya namna bora ya kutoa huduma tabibu za kifamasia.
Alhamisi ya Leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na shoka kwenye Europa League na Konferensi league ambapo michezo ya kwanza ya Nusu Fainali itapigwa. Suka mkeka wako sasa na meridianbet.

Mechi kali kabisa kwenye EUROPA leo itakuwa ni hii hapa ambayo inawkautanisha kati ya AS Roma dhidi ya Bayer Leverkusen ambao hawajapoteza mechi yoyote kwenye mashindano yote msimu huu, huku tayari wakiwa ndio mabingwa wa ligi kuu ya Ujerumani. Roma yeye anashika nafasi ya tano kwenye ligi hadi sasa baada ya kucheza mechi zake 34.

Kwenye hii nusu fainali ya kwanza ambayo itapigwa katika dimba la Stadio Olimpico Meridianbet wao wamempa nafasi kubwa ya kuondoka na ushindi Alonso na vijana wke kwa ODDS 2.06 kwa 3.47. Je wewe beti yako unaiweka wapi hapa?. Beti na meridianbet sasa.

Atalanta yeye atakuwa ugenini kusaka pointi tatu dhidi ya Olympique Marseille kutoka kule Ufaransa. Timu hii kule Ligue 1 ipo nafasi ya saba baada ya kucheza mechi zake 31 hadi sasa, Wakati vijana wa Gasperini wao wapo nafasi ya sita kwenye michezo yao 33 waliyocheza hadi sasa.

Mechi hii imepewa ODDS 2.55 kwa 2.69. Je nani kuondoka na ushindi leo hii kwenye hii mechi ya kwanza ya Nusu Fainali ambayo kila mmoja anaitamani sana kuvuka na kwenda fainali? Tengeneza jamvi hapa.

Ukiachana na mechi ndugu mteja kumbuka kucheza michezo ya Kasino ya Mtandaoni ambayo inatolewa ndani ya meridianbet kama vile Poker, Roullette, Aviator, Rockertman, Keno, Sloti na mingine kibao. Ingia mchezoni na ucheze sasa.

Vilevile michuano ya Konferensi Ligi nayo kama kawaida zitapigwa mechi mbili za maana kabisa ambazo hutakiwa kukosa nikianza na mtanange wa Aston Villa kutoka Uingereza dhidi ya Olympiacos Piraeus kutoka Ugiriki.

Villa ya Unai Emery ndio inapendelewa kuondoka na pointi tatu ndani ya Meridianbet kwa kupewa ODDS 1.37 kwa 8.23. Pia mechi hii ina machaguo zaidi ya 1000. Ingia meridianbet na ubashiri sasa.

Vilevile Nusu Fainali nyingine ni hii ya ACF Fiorentina dhidi ya Club Brugge ambao wapo nafasi ya pili kwenye ligi kuu ya Ubelgiji wakiwa wamepoteza mechi saba pekee hadi sasa. Huku Mwenyeji yeye akiwa nafasi ya 8 na akiwa amepoteza mechi 11 kwenye ligi.

1.73 kwa 4.60 ndio ODDS za mechi hii. Suka jamvi lako muda huu na uanze kubashiri mechi hii ili ujiweke kwenye nafasi ya kukwapua mpunga wa meridianbet.


Ingia katika ulimwengu wa zawadi za kushangaza: Jishindie sehemu ya zawadi zenye thamani ya Tsh Bilioni Moja (1,109,338,868) pale unapocheza michezo ya kasino ya mtandaoni kutoka kwa watengenezaji wa michezo ya kasino Wazdan.

Karibu katika ushindi usio na kifani! Burudika na Meridianbet unapocheza kasino ya mtandaoni na jishindie sehemu ya zawadi zenye thamani ya Tsh Bil 1 na bonasi za kasino kama zote. Kwa kujisajili na Meridianbet unakuwa na sifa za kushiriki kwenye promosheni hii kubwa Zaidi kwa sasa pale Meridianbet.

Meridianbet kwa ushirikiano na mtoa huduma Wazdan wamezindua promosheni ya kusisimua ambayo itadumu kwa miezi mitano! Kuanzia tarehe 29 Aprili hadi tarehe 29 Septemba, unapata fursa ya kujishindia sehemu ya zawadi zenye thamani ya hadi 1,109,338,868.

Wakati unacheza mchezo huu wa kasino ya mtandaoni labda wewe ndiye utakayekuwa na bahati na kushinda moja au zaidi ya zawadi za fedha zilizochaguliwa.

 Ikiwa unataka kuwa sehemu ya mchezo huu uliopewa jina la Mystery Drop, ni rahisi tu kuweka dau stahiki kwa sababu katika promosheni hii yenye michezo ya kasino ya mtandaoni hakuna vigezo vya chini vya dau kwa kila mzunguko.

Ili kucheza promosheni hii weka dau unalotaka, Jisajili, na cheza michezo ya kasino ya mtandaoni inayopatikana kutoka kwa mtoa huduma Wazdan.

Zawadi za pesa taslimu 100,000 zitagawiwa kwa wachezaji wenye bahati zaidi na ikiwa bahati itakuwa upande wako, unaweza kushinda moja au zaidi ya zawadi!


Top News